
Drafti la Tanzania kucheza mtandaoni
TZDraft ni jukwaa la mchezo wa draft (drafti / bao) mtandaoni lililotengenezwa kwa kufuata sheria za draft za Tanzania, kwa ajili ya Watanzania wanaopenda mchezo wa draft.
Lengo letu ni kumrahisishia kila mtu kucheza draft wakati wowote na rafiki yake au na wachezaji wengine wenye kupenda na kuthamini utamaduni wa mchezo wa draft, bila kujali mahali alipo, kwa kutumia simu au kompyuta.
Kupitia TZDraft, sasa unaweza kufurahia **online matching**, ambapo unacheza na wachezaji wengine moja kwa moja mtandaoni.
Unaweza pia **kucheza na marafiki zako online** kwa kuwaalika kwenye mchezo binafsi (private match) na kushindana pamoja bila kujali mpo wapi.
Pia tunafurahi kutangaza huduma yetu mpya — Mashindano ya Draft Mtandaoni (Online Tournaments).
Huduma hii itaruhusu wachezaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi kushiriki mashindano na kushindana ili kuwa mchezaji bora wa draft.
Sasa wachezaji wanaweza pia kuanzisha mashindano yao wenyewe, kuwaalika marafiki, na kupanga mashindano kwa urahisi.
Dhamira yetu ni kujenga jamii kubwa zaidi ya wachezaji wa draft mtandaoni nchini Tanzania.
Anza kucheza leo kupitia TZDraft na uwe sehemu ya mustakabali wa mchezo wa draft.